
It is almost a week now since controversial billionaire Jacob Juma was assassinated on his way home. The tragic ordeal has really provoked a lot of reactions from Kenyans but mostly instilled fear into the likes of Robert Alai,Cyprian Nyakundi and worse on the fearless investigative journalist,Mohammed Ali.
Honestly,Moha has triumphed over a test of times when it comes to death threats and the likes. His regular habit of rubbing off popular top government officials by exposing their dirty games has seen him on constant fear for his life. This is not the first time Moha is talking about a planned assassination on him,however this time,it sounds more intense.
Jacob Juma’s assassination seems like a message to people like him to mind their business and let the Who is Who be. Like Moha,the deceased had predicted his death several time and even boldly named the alleged perpetrators on his tweets.
Seems Moha is seeing death calling,this time more louder than any other time as the post below suggests;
“NIKIFA KESHO WENGINE WAJASIRI WATAZALIWA.
Huenda mada ya leo ikakutia hofu ama tumbo joto na kuwafurahisha wengine lakini usiwe na wasi wasi kwani kuzaliwa na kufa ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Nikifa kesho msilie wala msinung’unike. Nikifutwa kazi kesho msiwe na chuki na mtu yeyote. Nikifungwa jela kesho msilie maana hii ndio safari ya mwanadamu ya kila siku. Msilie maana tulipofika sasa kama taifa tutalengwa wachache tunaopinga dhulma za kila siku. Tutalengwa wachache wanaopiga vita dhidi ya ufisadi. Tutalengwa kwa sababu tumekataa kuabudu miungu midogo midogo inayozidi kubaka taifa hili. Tutazidi kulengwa kwa sababu tumekataa kula meza moja na wabakaji wa demokrasia. Leo hii waandishi wa habari wanakamatwa kiholela na polisi kwa sababu ya kufichua uhuni wa baadhi ya viongozi wanaojifanya watumishi wa wakenya ilhali tabia zao ni kama panya buku. Tabia ya kung’ata na kupuliza. Wanahabari wanaachishwa kazi katika njia isiyoeleweka kwa sababu ya kusimama imara na kupinga maovu ya serikali. Sisi tayari tumetia kichwa chetu maji kukabiliana na lolote lile litakalojiri kwa ajili ya kusimama na wakenya. Leo kila mmoja wetu aliye katika taaluma hii ni mlengwa. Aliye katika afisi za serikali na anayepinga ukabila na wizi wa mali ya umma analengwa. Wengi wetu tunalengwa na kuzimwa ki-talanta kupitia wahuni wachache wanaojifanya wakubwa ila wao hawana tofauti na wale wanaobaka taifa hili, kwani ufadhili wa senti haramu za kuwapotosha wananchi kupitia taarifa bandia ndio kazi zao. Lakini leo nina habari njema kwa wakenya. Msiogope maana riziki yatoka kwake Mungu. Msiogope maana Mungu ni mkuu. Msiogope kudai haki zenu, mali yenu na uongozi mnaotaka. Msiogope kufutwa kazi kwa sababu ya kuunga mkono mabadiliko ya kweli. Hakika wengi wetu tutaumia katika safari hii ya kutetea nafasi yetu katika awamu ya tatu ya ukombozi wa Kenya. Awamu ya kuwaondoa wahuni wote mamlakani pamoja na wabakaji wa demokrasia. Mwaka wa 2017 utakuwa kama mwaka wa 2002 wakati ambapo vugu vugu litazaliwa kusafisha Kenya upya. Kesho ndio hiyo siku. Kesho yetu sote ni 2017. Kesho ni mimba ambayo imetungwa leo na yapaswa kujifungua. Twatarajia kujifungua mtoto mzuri aliyetungwa na atakaeleta mabadiliko na wala sio starehe. Wakenya wana maono sasa na hakuna mtu yeyote atakayejaribu kusimama mbele ya vuguvugu la mabadiliko. Wakenya wanataka waheshimiwe na kulindwa na wala si kuibiwa kila kukicha. Wakenya wanataka uongozi bora. Uongozi huo hautapatikana kwa kuwatesa baadhi ya watetezi wa haki za binadamu, wanahabari na wanasiasa wa upinzani. Hii itakuwa ni kosa kubwa kuwahi fanyika kwani wote hawa wanayafanya haya kwa minajili ya ukenya ndani yao na wala sio tamaa. Safari ya mabadiliko imeanza na hakuna aliye na nguvu ya kuzuia wanayoyataka wakenya. Safari hii itakuwa ya kiu, mateso na machungu lakini hakika dakika ya mwisho sote tutashinda. Sote tutaungana na kusimama kama taifa. Wakuachishwa kazi wataachishwa, wakufungwa jela watafungwa, wakuuawa watauawa, wakuteswa watateswa lakini Kenya itasimama imara baada ya safari hii. Safari ya kutafuta demokrasia huwa chungu na iliyojaa mitihani. Hii ni safari waliopita watangulizi wenzetu kama vile marehemu Nelson Mandela, Mwalimu Julius Kabarage Nyerere, Jaramogi Oginga Odinga, Masinde Muliro, Martin Shikuku, Raila Odinga, JM Kariuki, Pio Gama Pinto, Tom Mboya, Field Marshal Dedan Kimathi miongoni mwa wakenya wengine wengi na mashujaa barani afrika. Safari ya dhiki iliyoishia kuzaliwa kwa vyama vingi vya kisiasa mwaka wa 1991 kabla ya kuwaweka wakenya huru na kuwapa demokrasia ya kuuliza na kujibiwa kinyume na demokrasia dhalimu ya enzi za Jomo Kenyatta, Daniel Toroitich Arap Moi na sasa serikali ya madotcom kama wasemavyo iliyotutoa kutoka umaskini hadi ufukara. Serikali inayotumia mabavu kwa kutueleza sisi wapiga kura eti ya kwamba watatutawala hadi mwaka wa 2032 pasi na kuona soni. Iwapo vitisho hivi vya hata kabla ya sisi kupiga kura si wizi basi ni nini? Unapowapata viongozi wenye damu moto na wakavu wenye kiu ya kupora mali ya umma, viongozi wa kujipiga kifua ya kutawala taifa basi jiandaeni maana mnaokaa nao meza moja ni sawia na fisi anayejifanya kuchunga kondoo kwa niaba ya mwenye boma. Mnaokula nao kwa jina la ukabila ni vipofu wabaya wanaoshika walaji wenza mikono wakikosa nyama. Msiogope kufa, msiogope kuteswa maana kila dhulma haikosi mwisho. Leo nimeanza kwa kusema nikifa kesho kwa sababu najua unyama unaopangwa, najua hila chafu zinazopangwa dhidi ya wanaharakati wanaofanya kila wawezalo kukomboa Kenya upya. Hila hizi zimekuwa hatari kwa usalama maana zinatumiwa kwenye wino za ofisi mbali mbali nchini. Kwa wale wanaotaka wengine wafe kwa ajili ya kupinga miungu na makatuni wao nasema poleni maana yote yatakwenda kwa mapenzi na kudra yake mwenyezi Mungu. Watoto wanazidi kuzaliwa na kila wanapokosa nafasi yao katika jamii wanazidi kuuliza masuali. Kenya sasa watoto wametapakaa kila mahala, hawana kazi, wanauawa ovyo ovyo, wana elimu lakini hawaheshimiwi wala kupewa kazi, wana utu lakini wanadharauliwa. Zamu ya kuitisha nafasi yao imefika. Zamu ya kutaka taifa lao imefika. Zamu ya kutaka kuongoza taifa kutoka mikono ya watapeli, wafisadi na wabakaji wa demokrasia na haki ya msingi ya wakenya kuishi imefika. Vijana sasa wanataka Kenya yao, vijana sasa wana kiu cha uongozi, vijana wanataka kuoa na kuwa na maisha bora, vijana hawa sasa wanataka kazi. Je, ni nani atasimama mbele yao na kupinga hazi zao? Kenya inalia, Kenya inataka usaidizi wa dharura, wakenya wameamka kutoka usingizi ya kikabila. Wakenya wanataka Kenya yao. Safari imeanza. Nikififa kesho msilie ila muendeleze safari ya ukombozi!
Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN.
Kuwasiliana naye: mali@standardmedia.co.ke, FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Instagram: @mohajichopevu, Twitter:
@mohajichopevu,” wrote Moha on his Facebook page-a letter that has raised questions than answers.
MUKAMI KANYI